Victoria ya Tamaduni Mbalimbali

Victoria ni mojawapo ya sehemu yanye jamii nyingi mbalimbali zilizoungana pamoja katika dunia. Tunatoka nchi zaidi ya 200, tunazungumza lugha au lahaja 260, pamoja na kufuata imani 135 tofauti.

Serikali ya Victoria husaidia jamii yenye umoja wa kitamaduniambapo kila mtu anaweza kushiriki katika jamii pamoja na kupata huduma bila kujali utamaduni, lugha au dini na historia zao.

Serikali ya Victoria inaweza kusaidia utamaduni wa jamii mbalimbali kwa:

  • misaada ya jamii kwa ajili ya matukio, vikundi vya wazee, msaada wa shirika, shule za lugha ya jamii pamoja na mipango mingine.
  • misaada ya miundombinu ya kujenga au kuboresha majengo na vifaa.
  • msaada kwa ajili ya mipango ambayo hukabiliana na masuala ya jamii ikiwemo ni pamoja na mahitaji ya makazi
  • juhudi za utamaduni pamoja na madhehebu mbalimbali ili kukuza uelewano wa utamaduni na kidini pamoja na kukuza maelewano ya kijamii.

Pia tunasherekea utofauti wetu kwa kufanya matukio makubwa ikiwemo ni pamoja na: Sherehe ya Chakula cha Jioni cha Mea wa Mji (Premier’s Gala Dinner), Wiki ya Utamaduni Mbalimbali (Cultural Diversity Week), Tamasha ya Utamaduni Mbalimbali ya Viva Victoria (the Viva Victoria Multicultural Festival) pamoja na Tuzo za Ubora za Utamaduni Mbalimbali wa Victoria (Victoria’s Multicultural Awards for Excellence).

Chimbua taarifa katika lugha yako

Events Calendar

There are no upcoming events at this time.

find more events here >